JUKUMU LA VIJANA NI ZAIDI YA KUTAFUTA PESA — NI KUJUA KUZIWEKA ZIKUE.
JUKUMU LA VIJANA NI ZAIDI YA KUTAFUTA PESA — NI KUJUA KUZIWEKA ZIKUE. Wengi wetu vijana tunajituma sana: tunafanya kazi, tunaanzisha biashara, tuna hustle kila kona... Lakini ni wangapi tunaweka akiba zetu mahali ambapo pesa zinaweza kukua kimkakati? Soko la hisa ni moja ya maeneo ambayo vijana wengi bado hawajalielewa vizuri, lakini lina uwezo mkubwa wa kutuondoa kwenye maisha ya kuishi kwa mshahara hadi mshahara. Soko la hisa sio kwa matajiri peke yao. Ni sehemu ambayo mtu yeyote anaweza kuwekeza kama una elfu kumi, hamsini, au laki moja. Unaweza kununua sehemu ya umiliki wa kampuni kubwa kama NMB, CRDB, Vodacom, au kampuni za kimataifa kupitia mifumo ya uwekezaji wa pamoja. Kwa nini uwekeze kwenye hisa? Fedha zako hukua zaidi kuliko benki: Badala ya hela kulala kwenye akaunti bila faida ya maana, kwenye hisa inaweza kukua kwa asilimia 10 au zaidi kila mwaka. Unakuwa mshirika wa kampuni kubwa: Unapomiliki hisa, unamiliki sehemu ya kampuni. Ukiona NMB inalipa faida au Vodacom ina...