"Je, Umejiandaa kwa Yasiyotarajiwa?"

Kipindi cha Vita ya Pili ya Dunia, dunia ilibadilika kwa kasi ambayo hakuna mtu aliyekuwa amejiandaa nayo. Uchumi uliyumba, mataifa yalianguka, na maisha ya watu mamilioni yakabadilika ghafla — si kwa sababu ya makosa yao, bali kwa sababu ya tukio kubwa lisilotarajiwa.

Katika kitabu The Psychology of Money, Morgan Housel anaeleza wazi jinsi matukio kama haya — ambayo hatuwezi kuyatabiri — yana athari kubwa kwenye maisha yetu ya kifedha. Na hapa ndipo akiba inakuwa silaha ya msingi ya kujilinda.

Kuwa na akiba ni kama kuwa na kinga dhidi ya maisha.
Haitakiwi usubiri dharura ndiyo uanze kufikiria akiba. Kama historia inavyotuonyesha, mabadiliko ya ghafla ni sehemu ya maisha — iwe ni kupoteza kazi, ugonjwa, mabadiliko ya soko au hata janga la kitaifa.

Kwa hiyo, swali ni moja tu:
Uko tayari kwa "vita" yako itakapotokea ghafla?

Ikiwa ungependa kuelewa kwa undani jinsi watu hufanya maamuzi ya kifedha, na kwanini kuweka akiba ni zaidi ya tu "kuhifadhi pesa", basi nakusihi usome


The Psychology of Money. Ni kitabu ambacho kimebadilisha maisha ya wengi — na naamini kitakusaidia pia.

📘 Ninacho nakala ya kitabu hiki kwa ajili yako. Kama unahitaji, niandikie DM au acha ujumbe hapa na nitakuelekeza jinsi ya kukipata.

Au nitafute whatsup no.0744048875

Jiandae sasa — kabla hujalazimika kijiandaa

Maoni